Watuhumiwa Jaycee Chan (kushoto) and Kai Ko (kulia).
Staa wa filamu wa siku nyingi, Jackie Chan.
MTOTO wa staa wa filamu wa Hollywood, Jackie Chan aitwaye Jaycee Chan anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Beijing, China baada ya kukutwa na gramu 100 za bangi.Jaycee Chan ambaye pia ni staa wa filamu kama baba yake alikamatwa Alhamisi iliyopita pamoja na staa mwingine wa filamu kutoka Taiwan, Kai Ko ambapo wote walipimwa na kubainika wametumia madawa ya kulevya aina ya bangi huku gramu 100 za madawa hayo zikikutwa nyumbani kwa Jaycee.
Kwa mujibu wa polisi nchini China, iwapo atakutwa na hatia, Jaycee anaweza kwenda jela miaka mitatu.
Jackie Chan amesafiri kuelekea nchini humo kuona jinsi ya kumnusuru kijana wake huyo.
0 comments:
Post a Comment