February 10 stori kutoka Shinyanga walikoweka kambi timu ya wekundu wa Msimbazi Simba wakisubiri mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya Stand United, zimeandikwa stori mpya kuhusu kiungo wa timu hiyo kufikishwa kituo cha polisi, kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto ameripotiwa kufikishwa kituo kikuu cha polisi Shinyanga.
Mwinyi Kazimoto amefikishwa kituo kikuu cha polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la MwanaSpoti Mwanahiba Richard, Kazimoto anayedaiwa kufanya kosa hilo kutokana na kudai kuwa mwandishi huyo aliwaandika vibaya kuwa wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya Prisons na Mbeya City walikuwa chini ya kiwango na wanapaswa wachunguzwe kwa maana ya kuwa wamepewa rushwa.
Mwanahiba Richard
Hivyo baada ya mazoezi ya Simba yaliofanyika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ndio inaripotiwa Kazimoto alitenda kosa hilo, bado Kazimoto na viongozi wa Simba hawajapatikana kuzungumzia chochote juu ya tuhuma hizo, Mwanahiba aliriripoti katika kituo cha polisi na kupewa hati ya mashitaka (RB) yenye namba SHY/RB/895/2016, fomu ya matibabu (PF3) kisha akapelekwa hospitali kwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment