MAAJABU YA KAGERA: Moto wa Ajabu Wateketeza Nyumba Tatu!


Baadhi ya vitu vikiwa vimeungua
KAGERA: Familia tatu ikiwemo ya Wilfrida Patrice katika Kijiji cha Omukagando Kata ya Mabira Wilaya ya Kyerwa mkoani hapa imejikuta katika wakati mgumu baada ya moto unaodaiwa ni wa ajabu kuteketeza nyumba zao tatu ndani ya siku nne.
 
Akizungumza kwa masikitiko mmoja wa wanafamilia ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa, tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita ambapo mama yao (Wilfrida) alikuwa amekaa nje ya nyumba hiyo na baada ya muda mfupi alishuhudia moshi mkali ukifuka kutokea ndani.
 
“Hatukuamini kwani moshi ulianza kutokea chumba cha watoto na baada ya muda mfupi, ukaanza kuenea nyumba yote kiasi cha kuunguza vitu vyote japo tulifanikiwa kuuzima baadaye kabisa,” alisema ndugu huyo.
Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa, baada ya siku moja, Wilfrida akiwa katika kikao cha Vicoba alishtushwa na taarifa ya nyumba ya jirani yake nayo ikiwaka moto.
“Ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa familia, kwani tukiwa katika wakati mgumu nyumba nyingine ya ndugu yetu ikaungua moto napo chanzo hatukijua. Jumatatu yake tena nyumba ya mdogo wetu ambayo ipo mtaa wa tatu kutoka hapa nayo ikaungua, pia chanzo hakikujulikana,” alisema ndugu huyo.
Ndugu huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa, matukio hayo yatakuwa yamesababishwa na mtu mmoja wa eneo hilo ambaye wamewahi kutishiana maisha.
 
Mama aliyeunguliwa na nyumba, Wilfrida
“Kuna siku huyo mtu aliweka vitu vyake kwenye shamba la mama (Wilfrida), kesi ikawa kubwa wakapelekana mbali sana. Tangu siku hiyo mtu huyo amekuwa akileta vitisho kwa mama kuwa, lazima amfanyie kitu kibaya na ndiyo tunayoyaona sasa,” alilalamika ndugu huyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Omukagando aliyejulikana kwa jina moja la Pastori alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hata na yeye aliwahi kupewa vitisho kutoka kwa mtu huyo kisa kuamulia kesi yao.
“Mtoto wangu mmoja alitumwa aje kuniambia kuwa niache kuendelea kuitetea hiyo familia iliounguziwa nyumba zao la sivyo na mimi atanifanyia kitu kibaya,” alisema Pastori.
Kwa sasa familia ya Wilfrida inaishi kwa msaada kwani haina makazi maalum.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment