"Joto la Bomobomoa” limezidi kuapanda
kwa Wakazi wa Dar es Salaam hususani wale wanaotakiwa kubomoa nyumba zao
zinazodaiwa kujengwa maeneo ambayo siyohalali.
Joto hilo limemkumba msanii maarufu wa
Bongo Movies, Wastara Juma ambaye nyumba zake mbili hivi karibuni
ziliwekewa alama ya X akitakiwa kuzibomoa.
Wastara aliyekuwa miongoni mwa mastaa
kibao wa Bongo movies, Bongo Fleva na tasnia nyinginezo nchini
alishiriki kwa kiasi kikubwa kupiga kampeni za uchaguzi wakati akikinadi
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika audio hapo chini, Wastara
amefunguka mazito kuhusu nyumba zake kuwekwa alama ya “X” kwa ajili ya
kubomolewa, huku akigusia kujitoa kwake kufanya kampeni ya kukinadi
Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuugua.
SIKILIZA MWENYEWE HAPA
0 comments:
Post a Comment