Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa nje ya eneo la kiwanda.
Wafanyakazi hao wakijikusanya kumsikiliza mmoja wao aliyekuwa akizungumza jambo.Taswira ya nje ya kiwanda hicho.Hali ilivyokuwa nje ya kiwanda hicho.
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho (aliyevaa fulana ya Yanga ) akiziliwa mara baada ya kutaka kwenda kufungua geti ili aweze kuingia, alizuiliwa na wenzake.Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakionekana kuzagaa nje ya kiwanda.
MAPEMA leo wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA TEXTILE MILLS LTD kinachotengeneza vitenge na Kanga kilichopo eneo la Tabata jijini Dar es Salaam walijazana nje ya kiwanda hicho kwa madai ya kuwa wanashinikiza kupewa mikataba ya ajira ya kudumu.
Kamera ya Global Publishers ilipopita maeneo iliwakuta wafanyakazi hao wakiwa nje ya kiwanda na kunasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio hilo.
Mmoja wa wafanyakazi hao alipotakiwa kueleza kisa cha kuwa nje badala ya kuwa ndani wakichapa kazi alisema wametoka nje kugoma kushinikiza kupewa mikataba ya kudumu.
Mwandishi wetu alijaribu kwenda kwenye geti la kuingilia kiwandani ili aweze kuonana na uongozi ili uzungumzie sakata hilo akakuta limefungwa na hata alipojaribu kugonga, hakufunguliwa.
NA DENIS MTIMA/GPL
Wafanyakazi hao wakijikusanya kumsikiliza mmoja wao aliyekuwa akizungumza jambo.Taswira ya nje ya kiwanda hicho.Hali ilivyokuwa nje ya kiwanda hicho.
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho (aliyevaa fulana ya Yanga ) akiziliwa mara baada ya kutaka kwenda kufungua geti ili aweze kuingia, alizuiliwa na wenzake.Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakionekana kuzagaa nje ya kiwanda.
Kamera ya Global Publishers ilipopita maeneo iliwakuta wafanyakazi hao wakiwa nje ya kiwanda na kunasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio hilo.
Mmoja wa wafanyakazi hao alipotakiwa kueleza kisa cha kuwa nje badala ya kuwa ndani wakichapa kazi alisema wametoka nje kugoma kushinikiza kupewa mikataba ya kudumu.
Mwandishi wetu alijaribu kwenda kwenye geti la kuingilia kiwandani ili aweze kuonana na uongozi ili uzungumzie sakata hilo akakuta limefungwa na hata alipojaribu kugonga, hakufunguliwa.
NA DENIS MTIMA/GPL
0 comments:
Post a Comment