Robin Rihanna Fenty ‘Rihanna’ (kushoto) na Beyonce Knowles ‘Beyonce’.
Na Hamida Hassan
HOUSTON, Marekani
KUNA madai kuwa mastaa wawili mahasimu,
Robin Rihanna Fenty na Beyonce Knowles wako katika mazungumzo na
waandaaji wa shoo ya Super Bowl ili wakikubaliana wafanye shoo angalau
kwa nusu saa.
Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la
Mirror imeeleza kuwa, mdau mmoja aliyefahamika kwa jina la Chris Matin
amefanya mazungumzo maalum na wasanii wote wawili kwa ajili ya shoo
hiyo.
“Chris na bendi yake wanatarajia kuwa na
wasanii kama Katy Perry na Madonna pamoja na wacheza shoo wake lakini
wameamua kuwashawishi wasanii hao ili kuwa na ‘sapraizi’ tofauti siku
hiyo,” ilielezwa.
Kama Chris atakuwa amefanikiwa kuwaunganisha mastaa hawa atakuwa amefanya kitu kikubwa kwani wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment