Na Hamida Hassan
Miami, Marekani
MWANAMITINDO Amber Rose hivi karibuni alionekana kwenye duka la madawa ambapo alienda kununua dawa za kumsaidia kupata ujauzito.
Sosi anayefanya kazi kwenye duka hilo
lililopo Miami aliweka wazi kuwa, baada ya Amber kufika dukani hapo
aliomba kupatiwa dawa za uzazi ambapo alipewa ziitwazo Clomiphene.
Sosi huyo aliweka wazi kuwa, dawa
alizonunua Amber hutumika kwa wanawake ambao wanapata tabu ya kupata
ujauzito hivyo huenda mwanadada huyo anajiandaa kupata mtoto wa pili.
Katika harakati hizo, Drake ametakiwa
kuwa makini kwa kutumia kinga kwani huenda akawa baba wa mtoto wa pili
wa Amber kwa sababu kwa sasa wanadaiwa kutoka kimapenzi.
0 comments:
Post a Comment