Hamida Hassan na Richard Bukos
MAJANGA! Bomoabomoa inayoendelea jijini Dar imemkumba msanii wa filamu, Wastara Juma aliyejikuta akizimia kwa mshtuko.
MAJANGA! Bomoabomoa inayoendelea jijini Dar imemkumba msanii wa filamu, Wastara Juma aliyejikuta akizimia kwa mshtuko.
Ndugu wa karibu wa mwigizaji huyo aliliambia Ijumaa kuwa hivi
karibuni Wastara aliwekewa alama ya X na maafisa wa ardhi katika nyumba
zake mbili zilizopo maeneo ya Tabata-Barakuda jijini Dar kuonesha kwamba
ziko kwenye eneo hatarishi.
Moja ya nyumba iliyowekewa X
STORI KAMILI
Ndugu huyo alizidi kudai kuwa, siku maafisa hao walipokuwa wanaweka
alama hiyo, Wastara hakuwepo nyumbani na alipofika alishindwa
kustahimili hali hiyo na kujikuta akizimia na kuzinduka mara
kadhaa.“Alipozinduka aliendelea kulia siku nzima, anasikitisha kwa
kweli,” alisema ndugu huyo wa karibu.
SIKU 10 ZAMPA MACHUNGU
Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa kilichowashangaza ni kupewa siku kumi za kuondoa vitu vyao hali inayowafanya wajiulize watavipeleka wapi kwani siku ni chache.
Ndugu huyo aliendelea kusema kuwa kilichowashangaza ni kupewa siku kumi za kuondoa vitu vyao hali inayowafanya wajiulize watavipeleka wapi kwani siku ni chache.
Alama ya X iliyowekewa nyumba hiyo.
“Unajua tumepatwa na mshtuko mkubwa kwani hata hivyo tangu tuishi
hapa hatujawahi kukumbwa na mafuriko ya aina yoyote, ukiuliza ni kwa
nini wameamua kufanya hivyo unaambiwa sehemu hatarishi, kiukweli hatuna
la kufanya tumechanganyikiwa,” alisema ndugu huyo.
IJUMAA MZIGONI
Baada ya ndugu kuelezea tukio hilo, Ijumaa lilifunga safari hadi Tabata-Barakuda, zilipo nyumba zake hizo na kuzungumza naye.
Baada ya ndugu kuelezea tukio hilo, Ijumaa lilifunga safari hadi Tabata-Barakuda, zilipo nyumba zake hizo na kuzungumza naye.
ASHINDWA KUNYANYUKA
Waandishi walipotaka kuonana na Wastara kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na suala hilo alishindwa kunyanyuka kitandani hivyo kulazimika kumfuata chumbani.
Waandishi walipotaka kuonana na Wastara kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na suala hilo alishindwa kunyanyuka kitandani hivyo kulazimika kumfuata chumbani.
AFUNGUKA, AANGUA KILIO
“Sijui nina nini jamani, serikali ingeniangalia ni juzi tu nimemaliza nyumba yangu, hapa nilipo natafuta hela nyingi tu niende kwenye matibabu ya mguu wangu sijapata linakuja hili ha! (analiaaa).
“Sijui nina nini jamani, serikali ingeniangalia ni juzi tu nimemaliza nyumba yangu, hapa nilipo natafuta hela nyingi tu niende kwenye matibabu ya mguu wangu sijapata linakuja hili ha! (analiaaa).
ATESWA NA FAMILIA
“Naifikiria sana familia yangu ni kubwa sijui nitaipeleka wapi na shida
niliyonayo nimechanganyikiwa, namuomba Mungu kiukweli,” alisema.
0 comments:
Post a Comment