Madereva wa Mabasi Ya 'Mwendo Kasi' Wapanga Kuigomea Serikali

Madereva wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wamesema watagoma kuendesha magari hayo kufuatia uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi usiokidhi mahitaji.
Baadhi ya mahitaji hayo ni mshahara mdogo wa shilingi laki 4 kwa mwezi tofauti na makubaliano ya awali ya shilingi laki 8.

Wakiongea na Eatv leo, madereva hao wamesema pia wameshangazwa na kitendo cha uongozi wa mabasi hayo kuwapa mkataba wa kazi bila ya kuwapatia nakala yake jambo ambalo wamesema ni kinyume cha taratibu za ajira.
Madereva hao ambao leo walikusanyika katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka kilichopo eneo la Kamata wamesema tayari walishatangaziwa malipo halisi kuwa ni shilingi laki 8 hivyo kitendo cha kusainishwa mkataba wa malipo ya shilingi laki 4 hawakubaliani nacho.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment