January 11 ndio ilikuwa siku ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutangaza washindi wa tuzo kadhaa ikiwemo tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ambayo ilikuwa inawaniwa na Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo. FIFA usiku wa January 11 Zurich Uswiss wamemtangaza mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kwa mara ya tano.
Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya 5 ya Ballon d’Or
Hii ni list ya washindi wa tuzo nyingine za FIFA kwa mwaka 2015
Golikipa: Manuel Neuer,
Mabeki: Thiago Silva, Marcelo, Sergio Ramos, Dani Alves
Viungo: Andres Iniesta, Luka Modric, Paul Pogba,
Washambuliaji: Neymar, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo.
Kikosi Bora cha mwaka
Kocha bora wa mwaka Luis Enrique wa FC Barcelona
Wendell Lira wa klabu ya Atletico Goianiense ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka
Mchezaji bora wa mwaka wa kike Carli Lloyd kutoka USA ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.
Zilianza kupigwa self wakati wa shughuli ya tuzo
Ronaldo akisalimiana na mke wa Lionel Messi anayeitwa Antonio pembeni Neymar.
Ronaldo na Messi
Carli Lloyd na Lionel Messi wakiwa na tuzo zao
0 comments:
Post a Comment