LEMBELI Amponda Rais MAGUFULI Kwa Kumtembelea SUMAYE Hospitali... Soma Alichokiandika Hapa

MBUNGE wa zamani wa Kahama kwa tiketi ya CCM kabla ya kuhamia Chadema,James Lembel ameibuka na kudai kuwa haikuwa na maana kwa Rais Magufuli kumtembelea Waziri Mkuu wa zamani Fredick Sumaye aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili wakati alikuwa katika uangalizi mzuri zaidi wa kidaktari tena akiwa anapatiwa huduma zote muhimu.

Badala yake,Lembeli ambaye alishindwa vibaya katika kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini.amesema kuwa ni vema Rais Magufuli angeenda kuwajulia hali wahanga wa bomoa bomoa ili kujua hali zao na jinsi ya kuwasaidia.
Hiki hapa chini ndicho alichokiandika: 
Ni vema kuona mgonjwa, ila ana wauguzi na kitanda kizuri. Inaleta maana zaidi kutembelea waliovunjiwa nyumba na dola ili kuona wanapolala kwa sasa na kuwashika mkono.
Posted by James Lembeli – Chadema on 11 Januari 2016
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment