Leticia Nyerere enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki
dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland
jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki..
Msiba upo DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.
Leticia aliolewa kisha kutengana na
mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo
walifanikiwa kupata watoto watatu.
Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mungu ailaze roho ua Marehemu mahali pema peponi,
0 comments:
Post a Comment