VIDEO&PICHAZ: Shuhudia ARSENAL Walivyoabishwa Kwa Kipigo Cha 4-0 na Kina WANYAMA


Baada ya michezo tisa ya Ligi Kuu Uingereza kupigwa Jumamosi ya December 26 siku ya Boxing Day, ulibakia mchezo mmoja ambao ulikuwa unachezwa usiku wa December 26. Mchezo ambao ulikuwa unachezwa usiku wa December 26 ni mechi kati ya Southampton dhidi ya Arsenal katika dimba la St Mary’s lenye uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki 30000.

Huu ni mchezo ambao ulikuwa unatoa nafasi kwa Arsenal kukaa kileleni mwa Ligi Kuu kama ingefanikiwa kupata ushindi, kwa Leicester City wanaongoza Ligi hiyo wamekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Liverpool. Hivyo kama Arsenal wangefanikiwa kuifunga Southampton basi wangekuwa mbele ya Leicester City kwa tofauti ya point moja.

Dimba la St Mary’s limeonekana kuwa gumu kwa Arsenal kwa imeshindwa kutoa hata sare na kujiwesha kuondoka na point moja, kwani Arsenal ilikubali kipigo cha goli 4-0 dhidi ya Southampton. Magoli ya Southampton yalifungwa na Cuco Martina dakika ya 19, Shane Long dakika ya 55 na 90 na Jose Miguel Fonte dakika ya 69. Hii ni mechi ya 4 kufungwa kwa Arsenal katika jumla ya mechi zake 18 ilizocheza msimu huu.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa December 26
AFC Bournemouth 0 – 0 Crystal Palace
Aston Villa 1 – 1 West Ham United
Chelsea 2 – 2 Watford
Liverpool 1 – 0 Leicester City
Manchester City 4 – 1 Sunderland
Swansea City 1 – 0 West Bromwich Albion
Tottenham Hotspur 3 – 0 Norwich City
Newcastle United 0 – 1 Everton
Video ya magoli ya Southampton Vs Arsenal
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment