Weekend hii itakuwa na headlines za urembo kwenye mataji mawili makubwa duniani, yani ni kwamba itashuhudiwa fainali ya Miss World ambayo itafanyika Dec 19 2015 ndani ya Sanya China, alafu siku inayofatia yani December 20 itakuwa ni fainali ya Miss Universe Marekani.
Tanzania ina mwakilishi kwenye stage ya Miss Universe 2015 Marekani ambaye ni mrembo mwenye umri wa miaka 19 tu, Lorraine Marriot… Moja ya vitu ambavyo mrembo huyu anaiwakilisha Tanzania kwenye Miss Universe ni pamoja na utamaduni wetu.
Hapa ninayo picha ya mrembo huyo kwenye vazi la ubunifu la Taifa ambalo limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar, vazi hilo limeitwa ‘Angel of Ivory’ likimaanisha mrembo Lorraine ni ‘Malaika wa Tanzania’ anayelinda Tembo wanaouawa kwa ujangili, na pia mkononi ana fimbo la kimasai ambayo ina rangi za Taifa.
Mrembo Lorraine Marriot
0 comments:
Post a Comment