Beyonce Knowles a.k.a Queen Bey
ni miongoni ya wasanii wenye majina makubwa sana kwenye ulimwengu wa
muziki duniani. Uwezo wake wa kuimba na kucheza kwa manjonjo on stage ni
miongoni mwa vitu ambavyo Beyonce anajulikana kuvifanya kwa ubora sana!
Ukiachana na ustaa wake kimuziki, Beyonce
anajulikana kama msanii anayevunja rekodi duniani na moja ya hizo
rekodi ni hi jamii ya inzi ambayo pengine stori yao imeshawahi kukufikia
lakini kama hujawahi kuisikia, basi leo ningependa kuisogeza kwako
stori yao na staa huyo wa muziki
Beyonce Knowles.
‘Scaptia beyonceae’ ni jamii ya inzi inayopatikana Queensland, Australia na licha ya kugundulika na watafiti wa kisayansi mwaka 1981 inzi hao hawakuwahi kutafsiriwa kisayansi mpaka mwaka 2011 ambapo sehemu kubwa na muhimu ya jina lao limetokana na jina la Beyonce Knowles staa wa muziki wa Marekani! Ilikuaje? Ipokee hii.
Scaptia beyonceae.
Kwenye ripoti iliyotolewa juu ya jamii hiyo ya inzi miaka michache iliyopita, Mtafiti Bryan Lessard kutoka kwenye taasisi ya CSIRO iliyopo Australia alisema mara ya kwanza kwa inzi hao ‘Scaptia beyonceae’ kugundulika ilikuwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na jina la pili linalokamilisha jina lao la kisayansi ‘Beyonceae’ limetokana na uzuri wa maumbo ya matumbo yao kufananishwa na umbo la Beyonce…
>>> “Hawa inzi wana rangi fulani ya dhahabu inayopendeza kwenye umbo lao la chini, yani kuanzia tumboni kwenda chini na kwa kuwa hakuna aliyewahi kuwapa jina tukaona bora tuwaite ‘Beyonceae’ kama heshima kwa Beyonce kwani pia ilikuwa mchezo wa kawaida kwetu kutumia mfano wa umbo la Beyonce kuwatambua hawa inzi wakati bado tunahangaika kuwatafutia jina la kisayansi…” <<< Bryan Lessard.
Kama ilikuwa haijakufikia basi ipokee hii kwa mara ya kwanza mtu wangu!

0 comments:
Post a Comment