Kichwa cha TAMBWE wa YANGA SC ni Noma!

AmissTambwe2Straika wa Yanga, Amissi Tambwe.
Sweebert Lukonge,Dar es Salaam
STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe ni hatari kwa kufunga kwa kichwa, kwani katika mabao 43 aliyofunga kwenye ligi kuu tangu atue nchini, 21 ni ya kichwa.


Katika mechi ya juzi Jumamosi, Yanga iliichapa Mbeya City mabao 3-0, ambapo mawili kati ya hayo yalifungwa na Tambwe.Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema kuwa mabao 22 yalibaki alifunga kwa kutumia miguu yote miwili.

“Namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema inayonifanya nizidi kufanya vizuri katika kazi yangu ya soka ambayo ndiyo inayonipatia mkate wangu wa kila siku.
“Hata hivyo, tangu nimefika hapa nchini kuna rekodi nyingi nimeziandika ambazo najua watu wengi hawazijui ila nawashukuru Championi kwa kuwa makini zaidi na kazi yenu kwani wiki iliyopita mlipoandika kuwa nina zaidi ya hat- trick 20 wengi walishangaa lakini huo ndiyo ukweli,” alisema Tambwe na kuongeza:
“Hata hivyo nina rekodi nyingine ambayo wengi hawaijui kwani tangu nifike hapa nchini nimeshafunga mabao 43 katika mechi za ligi kuu mpaka sasa, mabao 19 nilifunga nikiwa Simba, 14 msimu uliopita nikiwa na Yanga na 10 ni ya msimu huu ambao bado unaendelea.

“Hata hivyo mabao 21 kati ya hayo nimefunga kwa kichwa, hivyo hiyo pia ni rekodi yangu nyingine ninayojivunia ambayo naamini hakuna mtu wa kuifikia kwa wachezaji wa sasa ninaocheza nao ligi kuu,” alisema Tambwe ambaye pia anaongoza kuzifumania nyavu kwa sasa akiwa na mabao 10, akifuatiwa na Elias Maguri wa Stand United mwenye mabao tisa.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment