Ni wazi sasa mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic hana mpinzani na atakumbukwa kwa muda wote kutokana na rekodi yake aliyoiweka muda wote, tuliwahi kusikia kuwa mashabiki wa soka wa Sweden kutokana na kumpenda na kumuheshimu Zlatan Ibrahimovic mashabki wa soka Sweden wangependa kumuona sura yake ikiwa katika hela ya nchi hiyo (Krona) sema sheria hairuhusu.
Zlatan ametangazwa kwa mara nyingine tena kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Sweden na kupewa tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya tisa mfululizo, kwa ujumla Zlatan Ibrahimovic ametwaa tuzo hiyo mara kumi na kwa mara ya kwanza alitwaa tuzo hiyo mwaka 2005 na mwaka 2007 ndio alianza kutwaa mfululizo.
Hii ni rekodi ya wachezaji wa Sweden waliowahi kutwaa tuzo hiyo kuanzia mwaka 2000 – 2015
0 comments:
Post a Comment