Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza anayekipiga katika klabu ya Manchester United ya Uingereza Wayne Rooney usiku wa November 9 alihudhuria pambano la mieleka. Rooney alihudhuria pambano hilo akiwa pamoja na mtoto wake wa kiume Kai.
Katika pambano hilo la WWE lililofanyika jijini Manchester usiku wa November 9 lilikuwa ni maalum na Rooney na mwanae pamoja na Wade Barret ambaye ni mchezaji wa mchezo huo alipigwa kibao na Rooney na kuanguka chini baada ya kutoa kauli za kejeli kwa Rooney wakati akiwa ulingoni na baadae kushuka nje ya ulingo na kumfuata Rooney.
“Katika
ulingo huu kuna wanaume wawili ndio wanahadhi ya Ubingwa lakini sio
Wayne Rooney wa Manchester United lakini unaweza panda ulingoni na
ukapigana kama mwanaume na namchukia huyo mtoto wako ambaye atamshuhudia
baba yake akishindwa” >>> Wade Barret
Baadae Wade Barret alishuka ulingoni na kumfuata Rooney alipokuwa amekaa na Rooney kumchapa kibao na kuanguka chini huku watu wakishangilia. Baada ya pambano kumalizika Wade Barret alitweet na kusema kuwa kesho anaenda Old Trafford kukutana na staa huyo sambamba na waandaaji WWE kumshukuru Rooney kwa kushiriki katika pambano hilo na kuwafanya watu wafurahi.
Video ya Wayne Rooney akimchapa kibao Wade Barret
0 comments:
Post a Comment