Akizungumza na Bongo5 leo, Bella alieleza sababu ya kwanini wimbo huo umeshindwa kufanya vizuri kama ilivyotarajiwa ukilinganisha na ukubwa wa wasanii waliomo.
Ngoma bado haina mzunguko kusema kweli, kwa sababu ilitambulishwa redio moja tu na bado haijakaa bado kwenye promotion,amesema.
Ngoma ni nzuri na itafanya vizuri, kwa sababu kuna ngoma nyingine inatambulishwa inafanya vizuri kwa siku za mwanzoni halafu inapotea lakini hii nina uhakika itafanya vizuri kutokana na muziki mzuri tulioimba.
Ngoja video itoke halafu watu wanajua nazungumzia nini kwa sababu mapokezi ni mazuri na watu wanahitaji kinachohitajika ni promotion tu.
Pia mimi wakati wimbo unatambulishwa sikuwepo, kwahiyo mimi naona ni promotion na wiki ijayo tunapokea video, aliongeza.
0 comments:
Post a Comment