Akaendelea kusema kwa sasa amekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitatu lakini tatizo hilo linaendelea ingawa mke wake hajui jambo hilo linavyomsumbua. Kinachotokea ni kwamba anapokuwa peke yake ndani ya nyumba peke yake huangalia picha hizo na kuanza kupiga punyeto, ingawa alidhani angeacha mara tu baada ya kuoa.
Athari alizopata kwa kuendekeza tabia hizo ni kukosa hamu kufanya tendo la ndoa na mkewe wakati mwingine hivyo kuna wakati anapata ugomvi na mkwewe akidhani kwamba anakwenda nje ya ndoa. Aliandika habari yake ili aweze kupatiwa msaada namna gani ya kuondokana na tatizo hilo. Kutokana na mtaalamu huyo ambaye anashauri watu ambao wameangukia kwenye tatizo hilo ni kwamba tabia hizo zinaweza kukuharibia ndoa yako kabisa kama uko miongoni wa waathirika.
Hakuna jambo ambalo unaweza kuliacha kirahisi kama umezoea kufanya kwa muda mrefu, kubadili tabia mbaya kunahitaji nguvu ya ziada kujitoa na wewe mwenyewe kutumia juhudi kubwa kuhakikisha unaacha kabisa.
ATHARI ZA PICHA NA VIDEO ZA NGONO
Si rahisi kuacha ila unahitaji kutumia muda mwingi ukiwa na mkeo vilevile kujadili jambo hilo kwa pamoja ili kupata msaada kutoka kwake. Vile vile unahitaji kuepuka kukaa peke yako bila kazi yoyote ya msingi ndani ya nyumba ili kufuta mawazo ya kufanya punyeto au kuangalia picha za ngono.
Jadili na mkeo ili muweze kupata suluhisho la kudumu, mjulishe kwamba umekuwa na shida hiyo ili kuokoa ndoa yako ingawa unahitaji lugha nzuri ya kuleta mada hiyo mezani. Mke anaweza kukusaidia kutatua suala hilo kihisia na kimwili na kwamba anahitaji kuwa na wewe kwa ukaribu zaidi ingawa juhudi kubwa inakubidi wewe mwenyewe kudhamiria kwa dhati kabisa kuondokana na tabia hiyo mbaya.
Watu wengi ni waathirika wa vitendo hivi ambavyo wengine waliingia kwa mkumbo hasa shule za boarding wakajikuta wanafanya kama sehemu ya maisha bila kujua madhara yake siku za usoni. Ni wakati umefika kwamba jamii na vijana kujua kila tabia mbaya ambayo unaiingiza kwenye maisha yako ni rahisi sana kuianza lakini kuiacha ni vigumu na itakugharimu sana. Unahitaji hekima ya kutosha kuanza kupambana na vitu ambayo havina tija kwenye maisha binafsi.
0 comments:
Post a Comment