WAREMBO HAWA SANAA IMEZAA MAJINA YAO!

 Video Queen, Agness Gerald.
KATIKA ulimwengu wa sanaa ikiwemo ya muziki na filamu, mashabiki wamezoea kuwaita mastaa f’lani kwa majina wanayotumia katika kazi zao ambapo majina hayo yamekuwa maarufu na yale halisi waliyopewa na wazazi wao yakisahaulika kabisa.
Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula.
Katika makala haya tutakuletea orodha ya mastaa ambao majina waliyotumia kwenye nyimbo au filamu yamekuwa ni maarufu kama ndiyo halisi wakati wana majina waliyopewa na wazazi wao.MASOGANGE Huyu ni Video Queen wa video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, jina halisi alilopewa na wazazi wake ni Agness Gerald.

Jina la Masogange lilikuja baada ya kushiriki kwenye video ya Wimbo wa Masogange ambao umeimbwa na Mbongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ hivyo kuanzia hapo limekuwa ni jina maarufu ambalo mashabiki wameshalizoea kama lake halisi. Johari Huyu ni staa wa filamu Bongo, jina lake halisi ni Blandina Chagula.

Johari lilikuwa maarufu baada ya kucheza filamu iliyokwenda kwa jina la Johari ambayo ndiyo imemfanya ajulikane ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Binti Kiziwi Mwanadada huyu ambaye ni Video Queen jina lake halisi ni Sandra Khan kwa sasa anatumikia kifungo nchini China kutokana na kukutwa na madawa ya kulevya jina hili la Binti Kiziwi alilipata baada ya kushiriki kwenye wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Z-Anto unaojulikana kwa jina la Binti Kiziwi.

Video hii ambayo ndiyo chimbuko la jina la Binti Kiziwi ndiyo ilimtambulisha mwanadada huyu kwa mashabiki na jina kuwa maarufu mpaka leo.
Shumileta Ni staa wa filamu Bongo Movies ambaye kwa sasa anaishi nchini India, jina alilopewa na wazazi wake ni Jennifer Mwaipaja.Jina la Shumileta alilipata baada ya kucheza filamu iliyojulikana kwa jina la Shumileta akiwa kama mhusika mkuu na hapo ndipo jina hilo lilianza kuwa maarufu mpaka sasa wengi wanamfahamu kwa jina hilo.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment