MREMBO SHTUKA! MUME HASUSIWI, UKISUSA ATAHAMIA HUKU....!

Asalam alaikum wapendwa wasomaji, mimi ndiyo mimi, Aunt Nasra Shangingi Mstaafu ukiuona ukurasa huu jua somo linakuja, tena somo haswaaa hivyo kuwa makini.

Kwa nini uchukuliwe mume na wewe upo ndani? Utasikia oooh mume siku hizi harudi nyumbani, sijui anakoroma akipanda kitandani, unatoa tu siri bila kuuliza, hujui kama wewe ndiyo chanzo cha yote kwani ulianza kumchokoza mume, kwa hilo sasa nakufungua bibi, endelea kuisoma namba kwa mambo ya kujitakia mwenyewe.

Mwanamke ulikuwa ukirukaruka, ukiombwa unyumba unasingizia tumbo, mara umechoshwa na watoto, mara nyonga zinauma sasa Shangingi Mstaafu nakujuza mwanaume haoneshwi jeuri bibi, anapewa kitu roho inapenda, ukilegea anahamia kwa wengine kwani wapo wengi wenye uhitaji.

Wapo watu wanaopenda kulalamika kuwa mume amemuacha amemchukua jirani yake au amemchukua rafiki yake, hivi huoni aibu mume kukushinda na kwenda huko unakolalamikia, kwa nini usijiulize kabla ya kulalamika?

Je, unamtiaje aibu somo aliyekufunda wakati unaolewa, huoni kama hufai kuitwa mke wewe unakubali vipi kunyang’anywa tonge wakati ulishaliweka mdomoni?

Sasa basi nikupe siri yangu, mwenzako mume wangu mpaka leo ananihusudu kwa sababu tu ya mambo ninayomfanyia, hata akinikosea nikiona nimemwambia na somo hajaelewa, huwa narudi chini na kumvumilia na baada ya hapo natafuta siku akiwa ametuliza mzuka wa hasira, nakaa naye chini, naongea naye taratibu. Hii yote ni sababu sipendi kumpa nafasi ya kutafuta kasoro zangu na kwenda kwa mtu mwingine.

Unajua mume hasusiwi, ukijaribu kumsusia anaenda kwa wenye kujua kudekeza na kubembeleza, mume ni kama mtoto shoga, unatakiwa kujipinda kuhakikisha unamlea na usimuache.

Wapo wanawake wanaoona bora liende, mume akija juu naye anakuja juu, akinuna naye ananuna na kuendelea na mambo yake.

Wanawake wenzangu wanaume wengine hutafuta sababu ya kwenda kwa vimada vyao, hivyo kununa kwako ndiyo furaha yake, nakusihi kama unaipenda ndoa yako fuata hayo niliyokwambia.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment