Somo langu si kubwa sana lakini ni la Muhimu sana kwa wasichana wanao jiheshimu na kutaka kulitunza Hekalu takatifu, (mwili ulio umbwa na kubarikiwa na Mungu mwenyewe.
Chumbani ni sehemu ya Siri, ambayo inamfanya mtu ajitawale na kufanya matendo ambayo nje mble ya hadhara hawezi kuyafanya, ikiwemo na kuvua nguo, kujaribisha nguo, kulala ukiwa mtupu kwa kujiamini, na kufanya lolote ambalo mbele za watu utaona Aibu.
Lakini sasa nimeona mambo ya chumbani yanafanyika hadharani kwa kutupa picha za video na mnato kwenye mitandao sijajua kwa maana gani ila mambo hayo yanawaweka watu Fulani Fulani kwenye utata sana hasa Dada zetu.
Picha za utupu.
Mimi naamini kuwa Picha hizi hupigwa kwa usiri mkubwa lakini utunzaji wake si wa Siri tena. Laptops na simu zetu za mikononi, ndio zinazo waumbua wengi sana, hasa zinapo haribika, na kuhitaji kupeleka kwa mtaalamu atengeneze.
Sababu kubwa alipiga picha wakiwa watupu na mpenzi wake, na mwisho wasiku zile picha zika vuja na kupeekwa mtandaoni, na zingine kusambaa kwenye simu za watu.Ushauri wangu.
Wasichana msikubali kupiga picha za utupu, kwasababu zinaudhalilisha uanamkewako na kukuvunjia heshima maisha yako yote. Kwani kitu kikisha ingia mtandaoni, hakitoki. Labda admin aamue kukitoa. Na Watu wanatabia ya kushare, hata mmoja akitoa, wengine wanakuwa wamesha download, na kuweka kwenye mitandao yao, hicho ndicho kibaya zaidi
0 comments:
Post a Comment