Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bronxy, Alma Salum akiwa na
Finance Manager, Isaya Christopher wakiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani).
Staa wa Ngoma ya My Woman My Everthing, Patrick Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’.
STAA wa Ngoma ya My Woman My Everthing, Patrick Nnaemeka Okorie
‘Patoranking’ anatarajiwa kuangusha bonge la shoo la kihistoria Novemba
27, mwaka huu ndani ya Fukwe za Escape 1, Mikocheni jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana huu, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Broxy Entertainment ambao ndiyo waandaaji wa shoo hiyo, Alma
Salum alisema kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kwa staa huyo kutua
katika jiji la Dar baada ya kufunika katika shoo ya Fiesta msimu
uliopita.
“Tumeamua tuwape burudani ya funga mwaka mashabiki wote wa muziki nchini
na kila mtu anajua kwa sasa, Patoranking ndiyo habari ya mjini kila
kona kutokana na kukubalika na nyimbo zake kama vile My Woman, Daniella
Whine na nyingine nyingi.
“Awali ilikuwa tumlete Tekno Miles lakini kutokana na kuwa na shoo tarehe hiyohiyo tuliokuwa tumepanga ikabidi tumchukue Patoranking,” alisema Alma.
“Awali ilikuwa tumlete Tekno Miles lakini kutokana na kuwa na shoo tarehe hiyohiyo tuliokuwa tumepanga ikabidi tumchukue Patoranking,” alisema Alma.
Alma aliongeza kuwa shoo hiyo itatambulika kama Friday Night Fever
ambapo mwaka huu kutakuwa na utofauti na shoo nyingine kubwa zote
zilizowahi kutokea nchini kutokana na staa huyo kufanya shoo ya mapema
na kisha kutakuwa na kitu kinachoitwa After Party.
“Listi kamili ya wasanii watakaomsindikiza Patoranking tutaitaja lakini
kwa sasa tunao wasanii kama vile Chibwa na Young D na niwaambie tu
ratiba kamili ya kutua kwa Patoranking itakuwa Novemba 25, mwaka huu
ambapo Novemba 26 atafanya ziara katika vyombo mbalimbali vya habari na
kisha Novemba 27, shoo rasmi itaporomoshwa Escape 1.”
Tiketi zitaanza kupatikanika kuanzia Jumatatu katika maduka makubwa
mbalimbali nchini kama vile Chid Mapenzi (Kinondoni), Bitebo
(Mwananyamala), Clouds na Escape 1 (Mikocheni) pamoja na vyuo vyote vya
jijini Dar kwa bei ya shilingi 15,000 kabla ya shoo na 20,000 mlangoni.
PICHA/STORI: ANDREW CARLOS NA MUSA MATEJA/GPL
0 comments:
Post a Comment