KHLOE KARDASHIAN AMUACHA LAMAR, AREJEA KWA MPENZI WAKE -PICHAZ

Khloe Kardashian akiwa na mpenzi wake wa sasa, James Harden.

Khloe akiongozana na James Harden mwezi Septemba.
Los Angeles, Marekani
UBUYU mpya umepenyezwa kuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Khloe Kardashian, wiki iliyopita aliamua kumtelekeza aliyekuwa mumewe, Lamar Odom na kwenda kuhudhuria mechi ya NBA ambapo timu ya mpenzi wake wa sasa, James Harden, Houston Rockets ilikuwa inacheza.

Akichonga na mtandao maarufu wa burudani Marekani, mtu wa karibu kutoka katika familia ya Khloe alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano iliyopita na kuongeza kuwa, hata hivyo Harden alimpongeza Khloe kutokana na moyo wa huruma wa kumsaidia aliyekuwa mumewe huyo.

Mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Khloe Kardashian.
“Uhusiano wa Khloe na James unaendelea kama kawaida. Khloe anafurahia kurejea kwa mpenzi wake,” kilisema chanzo hicho.
Ikumbukwe kuwa kwa takribani wiki mbili, Khloe, 31, alikuwa akimpa sapoti Lamar ambaye ni mumewe wa ndoa lakini waliachana, aliyelazwa kutokana na kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya yaliyosababisha kupoteza fahamu kwa siku tatu.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment