No! Wakati supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
akiinjoi maisha kwenye hekalu lake lililoko maeneo ya Tegeta-Madale
jijini Dar, habari kutoka nyumbani kwa mama yake mdogo alikozaliwa na
kulelewa jamaa huyo Tandale zinadai kuwa choo cha nyumba yao kinamtia
aibu.
Choo cha nyumbani kwakina staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Habari kutoka kwa majirani waliokerwa na hali hiyo waliolipigia simu
gazeti hili zilieleza kuwa choo hicho cha nje kimeharibika, kujaa na
kutoa harufu inayohatarisha afya za wakazi wa mtaa huo kutokana na
ugonjwa hatari wa kipindupindu unaoenea kwa kasi nchini.
Akizungumza na waandishi wetu, mmoja wa majirani wa nyumba hiyo
maeneo ya Tandale-Shule, alisema kuwa choo hicho kiliharibika tangu
mwezi uliopita kwa ukuta wake kuangukia nyumba ya pembeni huku shimo la
choo likifumuka na kuacha uchafu wazi.
Waandishi wetu walishuhudia choo hicho kikiwa kimezungushiwa
manailoni huku upande wa chini ukionesha uchafu na harufu kali ikisambaa
eneo hilo huku jambo la kushangaza likiwa ni supastaa huyo na mama
yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ kufika mara kwa mara nyumbani hapo hasa
kila anaposhinda tuzo zake za kimataifa na kukikaushia choo hicho.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Issa Mnally na Brighton Masalu
0 comments:
Post a Comment