Ayodeji Ibrahim Balogun, maarufu kama Wizkid ni msanii ambaye kwasasa
wanamuziki wengi wakubwa wa Marekani, sio tu wanapenda muziki wake bali
wanatamani kumshirikisha katika kazi zao.
Akiwa Tanzania wiki iliyopita, Wizkid (25) aliwataja baadhi ya
wasanii wakubwa duniani ambao wametaka kufanya naye kazi, kumshirikisha
katika kazi zao.
Miongoni mwao alimtaja mfalme wa RnB, Robert Kelly ambaye alimpigia
simu na kumtumia wimbo wake anaotaka arekodi naye, wimbo utakaokuwa
kwenye album ya R.Kelly.
Msanii mwingine ambaye ameonesha kumkubali Wizkid ni Alicia Keys,
ambaye amempa shavu la kutumbuiza kwenye hafla ya kampeni yake ya ‘Keep A
Child Alive ‘ itakayofanyika Nov.5 jijini New York, Marekani. http://www.mwanalizombe.com/2015/11/baada-ya-kuonesha-kumkubali-wizkid.html
Kwa mujibu wa mtangazaji wa East Africa Radio, Sam Misago ambaye
alifanya naye mahojiano alipokuwa Dar, Wizkid amethibitisha kuwa baada
ya hafla hiyo ataingia studio na Alicia Keys kurekodi wimbo ambao
utakuwa ni wa Alicia Keys.
Hit maker wa ‘No One’ ambaye ni mke wa producer Swiz Beatz, alianza
kuonesha kupenda kazi za Wizkid miezi miwili iliyopita, kwa kupost video
Instagram akicheza nyimbo zake ikiwemo ‘Ojuelegba’.
0 comments:
Post a Comment