Wengi waliitafsiri post hiyo kama amelalamika kukosa tuzo za Afrima zilizotolewa Jumapili hii nchini Nigeria, licha ya kutajwa kwenye vipengele vinne.
Akiongea na kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM kufafanua kuhusu post hiyo ya Instagram iliyofutwa tayari, Kiba alisema aliamua kuandika hivyo kuwashukuru mashabiki wake kwa namna wanavyompigania na kuwahakikisha kuwa anajitahidi kwa nguvu zake zote kuwafurahisha lakini kuna mambo wasiyoyajua yanaendelea nyuma ya pazia.
“Sikuandika kwasababu ya tuzo, niliandika kutoa shukrani kwasababu walipiga kura lakini vile vile vitu ambavyo nafanyiwa mimi vingine sio vya kuvisambaza,” alisema.
Bongo5 imemtafuta mtu wa karibu kwenye uongozi wa Alikiba kutaka kujua kile ambacho wanahisi msanii wao anafanyiwa na wengi hawavijui.
Mtu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa Alikiba hafanikiwi kimataifa.
Ametolea mfano video za Mwana na Chekecha Cheketua pamoja na kuwa na viwango vinavyokubalika na kuongozwa na waongozaji mahiri barani Afrika, kituo cha MTV Base hakijawahi kuzicheza na wanapokuwa wakiuliza sababu wameshindwa kupewa maelezo yasioeleweka.
“Tunawatumia MTV Base, video wanazipokea na wanatuma confirmation ya kuzipitisha lakini hatuelewi kwanini hawazichezi tena,” amesema.
Amedai kuwa waliwapa Soundcity kipaumbele cha kucheza video ya Mwana kwa mara ya kwanza lakini baada ya hapo video hiyo haikuwahi kuchezwa tena.
“Hata zile Top Ten East yao haikustahili kuingia kweli? Kuna video ngapi za Afrika Mashariki zinaingia kwenye top ten na zingine ni za kawaida tu iweje Mwana isichezwe?” amehoji.
“Kinachoshangaza zaidi, kuna watu wanawaambiaga wasanii ukitaka kutoboa tobo kimataifa lazima upitie kwao.”
Kwa mifano hiyo amedai kuwa Alikiba anahisi kuna watu wanaofanya kila njia hata kwa kumwaga fedha ili kuhakikisha kuwa jitihada anazozifanya hazifiki popote na kwamba kitu hicho kinamnyong’onyeza sana.
Ametoa mfano jinsi ambavyo Alikiba anakubalika nchini Kenya anakopachukulia kama nyumbani pia.
Ametolea mfano wimbo wa Nagharamia alioshirikishwa na Christian Bella kuchezwa kwa zaidi ya mara 10 kwenye kipindi cha Classic 105 ‘Maina In The Morning’ kinachoendeshwa na Maina Kageni aliyewaambia kuwa hakijawahi kutokea kitu kama hicho kwenye historia ya show hiyo.
Kuhusu tuzo, amesema uongozi pamoja na Alikiba mwenyewe wameamua sasa kutojihusisha na na baadhi ya tuzo wanazohisi zina mrengo wa kibiashara zaidi.
“Ali ameamua kuweka focus yake zaidi kwenye muziki wake na mashabiki na sio tuzo,” amesema.
“Hafanyi muziki ili apate tuzo anafanya muziki kwa ajili ya mashabiki zake. Tuzo zitakuja tu by the way lakini sio his main focus. Why? Tuzo nyingi duniani siku hizi zinaanzishwa au zinaendeshwa kibiashara zaidi. Ni tuzo chache ambazo zimebaki kwenye misingi na zina credibility ya kueleweka. Kwa mfano tuzo zile Afrimma za US walimuweka kwenye kipengele cha upcoming, Ali ni legend. So unaweza kuona kabisa kwamba hawafutilii wanaweka tu watu ili tuzo zao zipate kiki,” amesisitiza.
“So alichoamua yeye baada ya kuzungumza na management kwamba from now on hatojihusisha kabisa na awards ambazo hazina credibility, ambazo zimeanzishwa au zipo kwa ajili ya kutumia wasanii kibiashara au kwa manufaa binafsi ya waandaji na sio kuwatuza kutokana na ubora wa kazi zao. Ali atashiriki kwenye awards lakini zile ambazo zina mrengo wa kuwatuza wasanii kwa ubora wa kazi na sio zenye mlengo wa kuwatumia kibiashara na mwishowe zinatengeneza vita/uhusiano mbaya baina ya wasanii.”
“Mfano mwingine ni hii Afrima ya Nigeria walimuweka kwenye categories ambazo hakustahili kama Album of the year? Ali hajatoa albam since 2009! Hizi zote zinaonyesha hawana umakini na wanafanya tu vitu kwa kukurupuka bila ufuatiliaji mzuri – hence no credibility.”
Pamoja na yote hayo Alikiba anadai anapenda watu wafahamu kuwa yeye si mtu mwenye kinyongo na mafanikio ya wasanii wengine na kwenye mahojiano na Diva aliwapongeza Diamond na Vanessa Mdee kwa ushindi wao.
“Wengi hawanijui tabia yangu lakini wanahisi labda mimi nina wivu ama nini. Hapana mimi nasupport muziki na nampenda kila mtu,” alisema Kiba.
0 comments:
Post a Comment