Staa wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba (kulia) kutoka Tanzania na Victoria Kimani kutoka Kenya.
Wasanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba kutoka Tanzania na
Victoria Kimani kutoka Kenya kesho Jumamosi watawasha moto katika
onyesho la muziki la Coke studio linalorushwa na luninga ya Clouds kila
siku ya Jumamosi.Ali Kiba ambaye anatamba na kwa vibao vyake mbalimbali katika msimu huu wa Coke Studio amefanya Kolabo matata (Mash- up) kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike maarufu kutoka nchini Kenya ,Victoria Kimani.
Wasanii wengine kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda, na wakati Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.
Alisema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii unatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema
0 comments:
Post a Comment