Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.
Khadija Mngwai,Dar es SalaamMSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, ameyakomba mamilioni ya Simba baada ya uongozi wa timu hiyo kukamilisha malipo yake ya zaidi ya shilingi milioni 14 aliyokuwa akidai baada ya kukatisha mkataba wake msimu uliopita.
Tambwe aliachwa Simba katika msimu uliopita kwenye dirisha dogo kufuatia kudaiwa kuwa, aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrick Phiri alimkataa katika kikosi chake kwa madai ya kushindwa kuendana na mfumo wake. Hata hivyo, Phiri alikanusha, akidai viongozi wenyewe ndiyo waliomkataa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe amesema kuwa, tayari ameshamalizana na Simba kwa kumlipa fedha zake zote kupitia mapato ya mlangoni, japokuwa ilikuwa tabu sana kupata malipo hayo.
“Ni kweli tayari nimeshamalizana na Simba kwa kunilipa fedha zangu zote nilizokuwa nikiwadai kutokana na kunikatishia mkataba wangu, japokuwa ilikuwa mbinde kunipa. “Kwa sasa siidai klabu hiyo na ninachoangalia ni jinsi gani naweza kuisaidia timu yangu ya Yanga iweze kufanikiwa kufanya vyema na hatimaye kutetea ubingwa wetu,” alisema Tambwe
0 comments:
Post a Comment