Mkali wa Hip Hop Ghana, Sarkodie.
Boniphace Ngumije
UWEZO ndiyo kigezo kikubwa kilichompa heshima Sarkodie kwenye medani
ya muziki wa Hip Hop Afrika ambapo tofauti na kujinyakulia tuzo 42 na
kuingia katika kinyang’anyiro mara 52, amekuwa akiandikwa katika chati
mbalimbali za burudani zikiwemo MTV, The Guardian, BET na E-TV ya Ghana
kuwa miongoni mwa wasanii watano wakali wenye heshima ya muda wote
barani Afrika.
Heshima yake ameijenga vipi?
Amejijengea heshima kwenye muziki wa Hip Hop hasa kutokana na kazi
zake kuwa zenye ubora unaokubalika katika tasnia hiyo. Mpaka sasa
amefanikiwa kutoa albamu nne zilizofanya vizuri kimauzo ambazo ni Makye
(2009), Rapperholic (2012), Darkology (2014) na Mary aliyoiachia mapema
mwaka huu.
Amewahi kuchukua mara kadhaa tuzo mbalimbali zenye heshima kubwa
duniani kama vile (MTV na AFRIMA) katika vipengele vya Msanii Bora wa
Hip Hop Afrika 2012 na 2013 na pia alikuwa msanii pekee wa Afrika
kushirikishwa kwenye michano ya Black Entertainment Television (BET)
maarufu kama Cypher mwaka 2012 pamoja na Talib Kweli, Jean Grae and
Ab-Soul.
Ujasiriamali na uwekezaji
Miongoni mwa mambo yanayomfanya mfalme huyu kutengeneza mkwanja mrefu ni
namna alivyojikita katika suala zima la ujasiriamali na uwekezaji akiwa
na hisa kwenye Kampuni ya Tigo, Ghana.Anamiliki Studio inayoitwa
Sarkcess Music, kituo cha kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira
magumu, maduka ya nguo yanayofahamika sana nchini Ghana, Sark by Yas
Clothing Line, ‘headphones’ zenye nembo ya Obidi na miradi mingine
mingi.
New Guy yazidi kumng’arisha
Kwa sasa mfalme huyu anabamba na Ngoma ya New Guy aliomshirikisha Ice Wood kutoka Marekani.
Ikumbukwe pia hivi karibuni aliachia ‘dokyumentari’ iliyoangaliwa sana na mashabiki wa muziki duniani kote kwenye Mtandao wa Youtube inayoitwa New Guy inayozungumzia na kuonyesha harakati alizofanya mpaka kufanikisha kurekodi Wimbo wa New Guy na msanii mkubwa Marekani, Ice Wood.
Ikumbukwe pia hivi karibuni aliachia ‘dokyumentari’ iliyoangaliwa sana na mashabiki wa muziki duniani kote kwenye Mtandao wa Youtube inayoitwa New Guy inayozungumzia na kuonyesha harakati alizofanya mpaka kufanikisha kurekodi Wimbo wa New Guy na msanii mkubwa Marekani, Ice Wood.
0 comments:
Post a Comment