Straika wa Stand United, Elius Maguli.
Nicodemus Jonas,Dar es SalaamSTRAIKA wa Stand United, Elius Maguli ambaye amekuwa na kasi nzuri katika ufungaji, amejinadi kuwa licha ya kutambua soka ni biashara, lakini kwake anaona bora asajiliwe na Yanga lakini hana mpango wa kurudi Simba.
Maguli ameliambia gazeti hili kwa mazingira ambayo yalimuondoa Simba, anaamini hayupo tayari kurejea klabuni hapo hata kama atahitajika na kusema bora atue timu nyingine yoyote, ikiwemo Yanga.
“Sawa, soka ni biashara lakini itahitaji muda kukaa chini kutafakari sana, lakini kama ni ofa kwa timu nyingine, poa, cha msingi ni masilahi na maelewano ya kikazi,” alisema nyota huyo wa zamani wa Ruvu Shooting.
0 comments:
Post a Comment