Mrembo, Happiness Wilfred Nassari (27) anayedai kushiriki imani ya kifreemason.
Stori: Chande Abdallah, Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani/Amani INATOSHA! Mrembo, Happiness Wilfred Nassari (27), ameibuka na kudai kuwa amekuwa akisali bila nguo kwenye ibada ya imani ya Freemason inayosifika kwa ushirikina.“Nilipojiunga ilikuwa si kwa matakwa yangu, kwani nilianza kwa kupata matatizo ya kuumwa magonjwa ya ajabuajabu, ikiwemo kutokwa na wadudu usoni kiasi cha kunitoa vidonda,” alisema mrembo huyo huku akionesha makovu ya vidonda hivyo.
“Hali ilipokuwa mbaya, ilibidi niende kwa mganga mmoja wa kienyeji ambaye aliniambia nimetupiwa majini ya kunuka ambayo yanabadilika harufu kila mara, lakini alitaka nimlipe shilingi milioni 5 ili anitibie, nikashindwa, nikaondoka.
alisema.
Moja ya alama za imani ya kifreemason.
Alisema baadaye alijikuta akiwa muumini mkubwa wa Freemason lakini si kwa hiari yake. Akaongeza kuwa, alipewa uwezo wa kusafiri mbali ya Tanzania kwa usiku mmoja na kukutana na wazungu ambao anaamini wana uwezo mkubwa wa mambo ya kiroho kuliko walokole wa siku hizi. “Hali hiyo ilifika mahali mpaka nikaanza kushirikishwa ibada zao kwa kusali bila nguo. Tulikuwa tunakwenda kwenye hekalu la ibada tukiwa tumevaa lakini tukifika ndani tunavua nguo na kubaki kama tulivyozaliwa na kuanza kusali. Hekalu hilo lipo hapahapa Dar es Salaam, lakini naomba nisiseme lilipo.
“Jambo kubwa ambalo nataka kulisema kwa leo, si kwamba nimeachana nao, bado nipo. Ila nimejikuta nikiwa sina amani kwa kuficha habari hizi.“Ninachojua hata hapa ninapozungumza na nyinyi wanajua kila kitu, kwani wananifuatilia bado kwa sababu walishanipa fedha kwa ajili ya mtaji wa biashara, lakini kusema ukweli sina amani,” alisema Happiness na kuanza kulia.
Alimalizia kwa kuweka wazi kwamba, kwa wale wanaotafuta utajiri kwa kupitia imani ya Freemason, anawashauri kuachana na akili hiyo kwani utajiri wao unakuwa na masharti mengi ikiwemo kuua ndugu wakiwemo wazazi.Mrembo huyo ataanza kusimulia hatua kwa hatua ya namna alivyokutana na Freemason mpaka alipo sasa. Pitia mtandao huu wiki ijayo.
PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
KARIBU TENA!
0 comments:
Post a Comment