MAJONZI TELE! YEMI ALADE AZUNGUMZIA KIFO CHA BABA YAKE!


Mwanamuziki Yemi Alade wa  Igeria akiwa na Diamond wa Tanzania.
Marehemu baba yake Yemi.
MWIMBAJI maarufu wa kimataifa wa Nigeria, Yemi Alade, amezungumzia kwa mara ya kwanza kifo cha baba yake aliyefariki wiki iliyopita. 
Msanii huyo wa kike aliyevuma kwa wimbo wa ‘Johnny’, alitoa kauli yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliandika: “Mungu ambariki. Mbingu imepata malaika mwenye thamani kubwa,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha ya baba yake.
Kuhusu mazishi ya mzazi wake huyo, Yemi alisema maelezo yatatolewa wakati muafaka.
“Asanteni sana kwa ujumbe wenu. Mipango ya mazishi itatolewa wakati ukifika,” aliandika staa huyo.

PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO. 
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment