7 PICHAZ: JIONEE MANCHESTER CITY ILIVYOCHAPWA 2-0 NA ARSENAL

Santi Cazorla akiifungia Arsenal bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti.
Santi Cazorla akishangilia na wenzake.
Straika wa Arsenal, Olivier Giroud (wa kwanza kulia) akiifungia timu yake bao la pili.
Olivier Giroud akishangilia bao hilo.
Aaron Ramsey wa Arsenal akiwatoka wachezaji wa Manchester City, Jesus Navas (kulia) na Fernando (kushoto) wakati wa mtanange huo.
Kipa wa Arsenal, David Ospina akishangilia ushindi wa timu yake pamoja na beki wake Per Mertesacker (kulia).
KLABU ya Manchester City imepokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa Etihad jijini Manchester. 

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya England, mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Santi Cazorla kwa penalti huku la pili likifungwa na Olivier Giroud kwa kichwa.Kwa matokeo ya leo, Manchester City imeendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 huku ikiwa na pointi 5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea wenye pointi 52. Asenal wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 39.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment