Baadhi ya wanafunzi kutoka katika sekondari mbalimbali jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja na Makam wa Rais Makam wa Rais Makam wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, pamoja na viongozi wengine, akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu wa pili Benjamin Mkapa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wengine waliohuduria mkutano huo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimpa zawadi ya kinyago Mwenyekiti wa vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, anayefuatilia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Vijana wanasayansi duniani wametakiwa kutoka na njia mbadala kupitia tafiti wanazofanya katika tasnia ya jiolojia ili zisaidie katika kuendeleza rasilimali duniani hususan barani Afrika na hatimaye ziweze kulinufaisha bara hilo na kuleta maendeleo endelevu.
Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akifungua mkutano wa tatu wa vijana wanasayansi duniani unaoendelea jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, vijana wanasayansi wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadililiko kupitia rasilimali mbalimbali zilizopo Afrika yakiwemo madini, mafuta , gesi asilia na rasilimali nyingine.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa azitaka nchi za Afrika kuwapa nafasi vijana.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya pili, Benjamin Mkapa amezitaka serikali za nchi za Afrika kuipa kipaumbele cha pekee elimu kwa vijana wanasayansi pamoja na kuwapa nafasi kuonesha na kutoa ufumbuzi kutokana na tafiti mbalimbali wanazozifanya ili kuweza kuziendeleza rasilimali zilizopo barani Afrika.
Profesa Muhongo aeleza Afrika ni bara la kizazi kijacho
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Afrika ni bara la kizazi kijacho, na kuongeza kuwa, vijana wanasayansi wanayo nafasi kubwa kuleta mabadiliko na kuendeleza rasilimali zilizopo Afrika kwa ajili ya kizazi kijacho.
Vilevile Profesa Mihongo amezitaka Serikali barani Afrika kuwekeza kwa vijana ili kuweza kupata wataalam waliobobea huku akitolea mfano Tanzania kuwa, dhamira ya Serikali kufikia mwaka 2025 ni kuhakikisha kwamba Tanzania inahesabika kuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati kupitia rasilimali za mafuta na gesi asilia. Hivyo uwepo wa wataalamu waliobobea katika taaluma hiyo ni muhimu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma, ameeleza kuwa, ni fursa nzuri kwa vijana kujifunza kutoka kwa wajiolojia waliobobea, jambo ambalo litawasaidi kufuata nyendo za wataalam hao. Ameongeza kuwa, kupitia uzoefu ambao vijana hao wataupata, utasaidia katika kufanikisha masuala mbalimbali ya kiuchumi na kuinua nchi zao kutokana na taaluma hiyo.
Vilevile, ametoa pongezi kubwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kuirithisha taaluma hiyo kwa vijana wa Tanzania, Afrika na duniani kupitia nafasi mbalimbali ambazo amekuwa kiongozi kupitia taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuongoza Wizara ya nishati na Madini.
Kwa upande wake Rais wa vijana wanasayansi duniani, Meng Wang, ameeleza kuwa hii ni nafasi kwao ya kuwasilisha tafiti uzoefu, changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Aidha, ameongeza ni fursa kwa Afrika ikizingatiwa kuwa, mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza barani humo.
0 comments:
Post a Comment