TABIA MBAYA: Ciara na Future wameachana na hivi sasa sio wapenzi tena.

Future amefuata tena historia yake ya kuwa na uhusiano,kupata mtoto na kutafuta mwanamke mwingine na hivi sasa amefanya hivyo kwa Ciara. Mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini hivi sasa zimekuwa rasmi kabisa kutokana na vyanzo vingi kuthibitisha habari hizi kutoka kwa Ciara.

Magazine ya Us Weekly limethibitishiwa habari hizi kutoka kwa mtu wa karibu na Ciara kwa kusema kwamba Future alimuongopea kwenye mapenzi yao na Ciara ameamua kuchukua njia yake na kuweka akili yake kwa mtoto zaidi.

Japokuwa lebo ya muziki inawafanya wawe karibu kutokana na kuwa ndani ya lebo moja, Ciara akikutana na Future ni kwa ajili ya kazi tu na sio uhusiano mwingine.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment