PIGO KUBWA BRAZIL...

STAA wa timu ya Brazil, Neymar hataendelea na michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuvunjika mfupa unaoshikana na uti wa mgongo wakati wa mechi yao na Colombia usiku wa kuamkia leo.
Neymar akitolewa nje ya uwanja wakati wa Robo Fainali dhidi ya Colombia.
Staa huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.
Neymar akiwa chini baada ya kuvunjika mfupa.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu.
Hivi ndivyo Neymar alivyoumia.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.
Wapenzi wa soka nchini Brazil wakiwa nje ya hospitali aliyopelekwa Neymar.
JE, UMEPITIA MAGAZETI YOTE YA LEO JUMAMOSI?!YAPO HAPA
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment