KUSHAMBULIWA KWA BASI LA MAGEREZA TANZANIA KATIKA PICHA...!

BASI la Jeshi la Magereza lililokuwa na mahabusu likitokea Mahakama ya Kawe jijini Dar es Salaam, limeshambuliwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki.Inadaiwa kuwa watu hao walitaka kumdhuru mtu aliyekuwa kwenye gari lililokuwa mbele ya basi hilo.
Walipoliona basi hilo wakadhani kuwa lazima kutakuwa na askari wenye silaha ndipo wakalishambulia. Katika shambulio hilo, dereva wa basi na askari mmoja wamejeruhiwa na hakuna mahabusu aliyetoroka wala kujeruhiwa.
 Kioo cha nyuma cha basi hilo kilivunjika chote baada ya kushambuliwa kwa risasi.
Maeneo ya vioo vilivyoshambuliwa kwa risasi katika tukio hilo
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment