Shabiki wa Uholanzi akiwa amevalia jezi yake ya rangi ya machungwa akiigiza namna Van Persie alivyofunga bao la kichwaWAKATI Robin van Persie anafunga bao bora la kichwa katika ushindi mkubwa wa mabao 5-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Hispania, hakujua kama amefanya kitu cha ajabu katika mashindano hayo....
Bao hilo la kichwa limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hususani Twita.
Mashabiki wengi wa Uholanzi wakiwa katika bustani zao kwa mapumziko, wanaigiza namna mshambuliaji huyo wa Manchester United alivyopaa juu na kupiga kichwa na kufunga bao la bora zaidi mpaka sasa..
Hispania walishinda kombe la dunia mwaka 2010 kwa kuwafunga Uholanzi kwenye mchezo wa fainali, lakini safari hii mambo yamekuwa balaa.
The flying Dutchman: Van Persie aliifungia Uholanzi bao la kusawazisha
Van Persie akikimbia kumfuata kocha wa Manchester United, Van Gaal ili washangilie bao hilo.
Kula tano: Van Gaal na Van Persie wakishangilia bao pamoja na wanatarajia kukutana Old Trafford baada ya kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment