Stori: OFM, WIKIENDA
Morogoro: Inauma sana! Kile Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, imenasa tukio baya katika kufanya kwake kazi baada ya kushuhudia ‘live’ mgonjwa akifa kwenye mapokezi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro huku manesi na wahudumu wakiingia matatani kwa uzembe.
Morogoro: Inauma sana! Kile Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, imenasa tukio baya katika kufanya kwake kazi baada ya kushuhudia ‘live’ mgonjwa akifa kwenye mapokezi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro huku manesi na wahudumu wakiingia matatani kwa uzembe.
Kabla ya tukio hilo la mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa muda mrefu
OFM imepokea kero juu ya mapokezi hiyo kuwa huwa kuna ucheleweshwaji wa
kupokea wagonjwa hata wale wanaohitaji huduma ya dharura (emergency)
hivyo kuamua kufanya uchunguzi kwa kuweka kambi na kubaini kuwepo kwa
ukweli wa kero hiyo.
Katika siku zake kadhaa za kuweka ‘patroo’ eneo hilo, OFM ilishuhudia
wagonjwa wakilalamika kucheleweshwa kupokelewa lakini hakukuwa na
madhara ya mtu kupoteza uhai hadi ilipotokea kwa Moshi Mwandeme (30),
mkazi wa wilayani Kilosa aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Wilaya
ya Kilosa akisumbuliwa na maradhi ya kubabuka mwili kwa kula samaki
waliomdhuru.
Muonekano wa hospitali hiyo.
Wakati OFM ikiwa kazini ilimshuhudia Mwandeme akifikishwa hospitalini
hapo akiwa mahututi baada ya uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa
kumpa rufaa ya kuletwa hospitalini hapo kwa gari la wagonjwa (ambulance)
la wilaya.
Bila kujionesha kuwa ilikuwa ikifuatilia tukio hilo, baada ya umauti
kumfika Mwandeme, OFM ilimpa nafasi mama wa marehemu, Khadija Abdallah
ili kusimulia kilichotokea huku akirekodiwa sauti.
Kwa mujibu wa mzazi huyo, walipofika mapokezi walikaa na mgonjwa wao
kwa zaidi ya saa moja bila huduma na kwamba walipomuuliza mhudumu wa
zamu, aliwaambia kitanda cha kubeba wagonjwa ni kimoja hivyo wasuburi.
Huku akiangua kilio mama huyo alisimulia:
“Tumesubiri kwa muda mrefu,
mwanangu alikuwa akilalamika maumivu, mimi na dada yake, Zawadi Kheri
na nesi tuliyekuja naye kutoka Kilosa, tulimshusha mgongwa kwenye
ambulance na kumpeleka mapokezi.
“Ulipita muda mrefu sana, nesi tuliyekuja naye alikwenda tena kwa
nesi wa zamu aliyekuwa mapokezi na kumwambia mgonjwa wetu amezidiwa
hivyo wamuwahishe kumpa huduma lakini nesi huyo wa mapokezi alimjibu
nesi wetu kuwa manesi wa vijijini washamba hawaelewi.
“Kauli hiyo ilimchefua nesi wetu na kujikuta akitokwa na machozi kwa
hasira. Wakati tunambembeleza nesi huyo ndipo mwanangu akakata roho
akiwa mapokezi na watu wakishuhuda.”
Hata
hivyo, baada ya kutokea tukio hilo, baadhi ya watu walimshuhudia
Mwandeme akifa walipiga kelele wakitaka kumshushia kichapo nesi huyo
aliyekuwa mapokezi.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo baya, ilibidi mwili wa marehemu uwekwe kwenye gari kurudishwa Kilosa kwa mazishi kwa kutumia ambulance iliyompeleka.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo baya, ilibidi mwili wa marehemu uwekwe kwenye gari kurudishwa Kilosa kwa mazishi kwa kutumia ambulance iliyompeleka.
Baada ya kuibuka kwa kashfa hiyo nzito katika kipindi hiki ambacho
Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inatumbua majipu katika taasisi
zake, OFM ilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Dk.
Rita Lyamuya ili kuzungumzia kashfa hiyo ambapo awali aliwaka:
“Hivi ninyi siku zote mnaandika mabaya tu ya hospitali yetu? Kuhusu
hilo tukio mimi ndiyo naingia ofisini sijapata taarifa hizo ngoja niende
mapokezi nikaulize, nitakutafuta baada ya saa moja.”
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Dk. Rita Lyamuya.
Saa moja baadaye, Dk. Rita aliwaita OFM ofisini kwake ambapo
ilipofika ilimkuta na timu ya watu wanne ambapo daktari huyo
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo:
“Baada ya kufuatilia nimegundua ni kweli kuna mgonjwa alifia mapokezi
lakini kwa mujibu wa nesi wa zamu, mgonjwa huyo hakukaa zaidi ya saa
moja pale mapokezi na hii inatokana na muuguzi kumhudumia mgonjwa wa
kipindupindu aliyetangulia kufika.
“Tunao uchache wa vitendea kazi lakini naahidi tukio kama hili halitatokea tena.”
“Tunao uchache wa vitendea kazi lakini naahidi tukio kama hili halitatokea tena.”
0 comments:
Post a Comment