Rais John Pombe Magufuli Jumatano Januari 7, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika mkutano huo Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Rais Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa Ikulu
Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.
Naye Jaji Warioba amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.
“Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo” Jaji Warioba.
Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu
0 comments:
Post a Comment