Msanii na mtayarishaji wa muziki wa ‘The Industry’ Nahreel amepandisha gharama za kurekodi muziki kwenye studio yake kutokana na ukarabati mkubwa alioufanya.
Nahreel ambaye mwaka 2015 ametengeneza hits kama ‘Game’ ya Navy Kenzo, ‘Nana’ ya Diamond, ‘Don’t Bother’ ya Joh Makini na nyingine nyingi, amesema kuwa kutokana na ukarabati alioufanya katika studio yake, ameona aongeze bei ili kuendana na gharama alizotumia.

“Ukarabati huu unaoendelea unafanyika kwa kiwango kikubwa sana, kuanzia mazingira hadi vifaa vya studio vimekuwa vya kisasa. Lengo ni kutengeneza ngoma kali na zenye ubora zaidi na kuhusu price za kurekodi track zimebadilika kidogo ila nisingependa kuweka wazi upande huo coz unaweza ukaletewa kazi kubwa na msanii au mtu yoyote ikawa hailingani na bei niliyoitaja,” amesema Nahreel.
0 comments:
Post a Comment