Rais MAGUFULI Naye Kaguswa na Ushindi wa Mbwana SAMATTA! Kayaandika Haya...

Jana Tanzania iliandika historia katika medali ya soka Afrika na duniani baada ya mshambuliaji Mtanzania anakipiga katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Samatta alitangazwa mshindi huko Abuja, Nigeria katika tuzo zilizowashirikisha mastaa mbalimbali wa soka Afrika.

Furaha ya Watanzania pia imemgusa Rais wa awamu ya tano John Magufuli ambaye ametuma pongezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Rais amemtaka Waziri Nape amfikishie salamu za pongezi mchezaji huyo na pia tuzo hiyo imemjengea heshima kubwa na kuleta heshima kwa wachezaji wa Tanzania.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi..

Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment