Hiki Ndicho Kinachomtia Hasira Louis Van Gaal Ndani ya MAN United


Kocha ambaye bado anatajwa kuwa siku zake zinahesabika kuendelea kusalia ndani ya Man United Louis van Gaal, amerudi kwenye headlines na kauli ambayo huenda imewashangaza wengi. Louis van Gaal amekuwa akikosolewa na wachambuzi wa masuala ya soka Uingereza pamoja na wachezaji wa zamani wa timu hiyo juu ya mfumo wanaocheza Man United kwa sasa.
Kumbe sio mashabiki na wachambuzi wa soka pekee ndio huwa wanaumizwa na namna Man United wanavyocheza soka kwa sasa, bali hata Louis van Gaal ambaye ni kocha wa timu amekiri kuboreka wakati mwingine kuona Man United ikicheza mchezo mzuri, Van Gaal anakiri kuwa zipo mechi za Man United ambazo huwa anafurahia na zipo ambazo huwa zina mkera na kumtia hasira.

“Kuna baadhi ya mechi za Man United huwa na furahia sana kuona namna ambavyo timu inacheza, mfano mechi yetu ya karibuni tuliyocheza dhidi ya Chelsea, ila kuna baadhi ya mechi huwa napata hasira sana, lakini hilo ndio soka lilivyo sio kila siku timu itacheza mpira mzuri” >>> Louis van Gaal
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment