Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
YANGA imeizidi kete Simba katika utitiri wa washambuliaji
baada ya usajili wa nyota wawili kwa mpigo; Paul Nonga na Issofou
Boubacar ‘Garba’ ambao umeifanya kuwa na jumla ya washambuliaji nane,
mmoja zaidi ya watani wao.
Safu ya mbele inaundwa na; Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Garba, Nonga,
Matheo Simon na Malim Busungu, wakati huohuo kuna viungo washambuliaji
Geoffrey Mwashuiya na Simon Msuva ambao pia wanao uwezo wa kufunga.
Akifafanua kiufundi zaidi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, benchi lilifikia uamuzi huo kutokana na wingi wa mashindano yanayowakabili, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf).
“Ukiangalia tuna michuano mingi ambayo inatulazimu kuwa na kikosi
kipana zaidi. Caf, ligi kuu, Kombe la FA na hapohapo Mapinduzi
inatusubiri siku chache zijazo.
“Hivyo lazima uwe na kikosi kipana ili kama ni kasi ya kushambulia kusionekane pengo michuano kwa michuano,” alisema Mwambusi.
0 comments:
Post a Comment