Stori zilianza kama tetesi na baadae mmoja kati ya mitandao ya Ulaya ikaripoti mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya KRC Genk Dimitri De Conde kuwa katika mipango ya kukamilisha usajili huo, December 24 kunatajwa kuwa kulikuwa na mazungumzo ya kina kati ya viongozi wa KRC Genk na mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi juu ya dau la uhamisho wa staa huyo.
December 25 Jamal Kasongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta amethibitisha mazungumzo kufanyika na kuwa katika hatua nzuri “Moise Katumbi jana alikuwa Ubelgiji kushughulikia hili suala lakini amerudi Lubumbashi na kumuacha mwanasheria wake aendelee nalo, kwa sasa wanavutana kuhusu ada ya uhamisho anayohitaji Katumbi ila kama wakikubaliana tumuombee mungu tu kijana January atacheza Ubelgiji” >>> Jamal Kasongo
0 comments:
Post a Comment