Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure.
Amesema kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na Umeme.
Pia amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa 40% hadi 50% huku akisisitiza zaidi kuendelea na Kampeni ya (Nyumba yangu, Maisha yangu) ili wananchi wawezi kumudu gharama za nyumba hizo.

0 comments:
Post a Comment