Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Tiffah ametakiwa kutofanya shoo kama ile kutokana na ile ya mwaka jana iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar kuandaliwa kwa kukiuka baadhi ya masharti.
“Jamani kwa taarifa nilizozipata kutoka Basata (Baraza la Sanaa la Taifa), zinadai kuwa, Zari kwa sasa hataruhusiwa kuandaa tamasha hapa nchini hadi pale atakapofuata kanuni za Basata.
“Inasemekana Basata wamemuwekea ngumu baada ya kuandaa tamasha lake la mwanzo huku akishindwa kufuata baadhi ya taratibu zinazostahili kabla ya kuanza maandalizi.

“Kwa sasa sijui kama Zari anaweza kuruhusiwa kuandaa tamasha kwani kipindi kile anaandaa Zari All White Party alikiuka baadhi ya mambo likiwemo kuanza kutangaza shoo kabla ya kupata ruhusa kutoka Basata.
Rais Dk. John Pombe Magufuli.
“Mbali na hilo, pia kuna shilingi laki 5 ambazo alipigwa faini
kufuatia kosa hilo hadi leo sina uhakika kama alilipa maana najua fedha
aliyolipa ni milioni moja na nusu tu ambazo ni gharama za kulipia shoo,”
alisema afisa huyo.Ili kusikia kutoka kwa Zari, Amani lilimpigia simu mzazi mwenzake Zari, Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah ambaye hakupokea na alipotumiwa meseji kwa simu ya mkononi, hakuijibu.
0 comments:
Post a Comment