Sababu 6 za Wanaume Kuwahi Kufika Kileleni -2

Wiki iliyopita niliishia kueleza namna mazoezi yanavyoweza kumpa nguvu mtu zitakazomwezesha kushiriki tendo la ndoa bila matatizo na ambavyo watu wasiokuwa na tabia ya kufanya mazoezi wanapokabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Leo nitaendelea na mada hiyo. 

Kukamia kupita kiasi 
Ni kawaida wanaume wengi kukamia tendo la ndoa na kuona kufanya hivyo ndiyo kujipa morali wa kushiriki tendo katika kiwango cha juu.
Dr. Abrahams James wa Saint Magreth Clinic iliyopo Washington DC katika andiko lake liitwalo `Sex and Fertility` la mwaka 2011, amesisitiza kwamba, wanaume kutofuatilia majarida /elimu au taarifa za mbinu mbalimbali za kumwezesha mwanaume kuchelewa kufika kileleni, huchangia kuendelea kwa tatizo hili kwa kizazi na kizazi na hasa kwa wanaume wa mijini ambao wengi wao miili yao haifanyishwi mazoezi kwa kazi zao au hata kwa kupanga muda.

Anasisitiza kwamba mwanaume anapopata ufahamu huu hupata hali ya kujiamini na hivyo kushiriki kikamilifu katika tendo la ndoa.


Ulaji mbovu ukiambatana na uzito kupita kiasi
Ulaji wa siku hizi hasa mijini ni mbovu kwa maana ya kwamba watu hujali rangi na ladha na si viini lishe vilivyomo na pia hawajali matokeo mabovu ya ulaji huo.

Nashangaza kuona wasomi wengi na watu wenye uwezo kifedha wakiongoza kwa ulaji mbovu unaosababisha pamoja na mambo mengine, kukumbwa na tatizo la wanaume kuwahi kufikia mshindo na kutoweza kuendelea mpaka saa nyingi au hata siku zaidi ya moja zipite.
Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya.
Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye mtandao huu.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment